1 Chronicles 23:6-17

6 aDaudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

Wagershoni

7Wana wa Wagershoni walikuwa wawili:
Ladani na Shimei.
8Wana wa Ladani walikuwa watatu:
Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.
9Wana wa Shimei walikuwa watatu:
Shelomothi,
Yaani Shelomithi; maana yake ni Mpenda amani.
Hazieli na Harani.
Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.
10Nao wana wa Shimei walikuwa wanne:
Yahathi, Zina,
Tafsiri zingine zinamwita Ziza.
Yeushi na Beria.
11Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.

Wakohathi

12 dWana wa Kohathi walikuwa wanne:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
13 eWana wa Amramu walikuwa:
Aroni na Mose.
Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele.
14 fWana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.
15 gWana wa Mose walikuwa:
Gershomu na Eliezeri.
16 hWazao wa Gershomu:
Shebueli alikuwa wa kwanza.
17Wazao wa Eliezeri:
Rehabia alikuwa wa kwanza.
Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
Copyright information for SwhNEN